SIMBA NA TUSKER NGUVU SAWA, JAMHURI ASHINDA

Simba sc jana usiku alitoa sare ya goii moja kwa moja na Tusker ya Kenya katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kundi A katika michuano ya mapinduzi.

Katika mchezo huo ulichezwa usiku katika uwanja wa Aman mjini Unguja, simba walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Haruna Moshi Shaaban (Boban) ktika dakika ya 18.

Goli hilo lilisawazishwa katika dakika ya 33 ikiwa ni baada ya sinba kupoteza nafasi katika dakika ya 30. Goli hilo la tusker lilifungwa na Khalid Aucho.


Katika mchezo wa awali wa kundi hilo uliochezwa jana ulishuhudia Jamhuri ya Pemba ikipata ushindi wa goli 2-1 mbele ya Bandari ya visiwani humo.

Kundi A linaongozwa na Tusker mwenye point 4 sawa na Simba sc inayoshika nafasi ya pili akizidiwa goli mbili tofauti ya kufunga na kufungwa., Jamhuri ya tatu ikiwa na pointi 3 na Bandari ya mwisho ikiwa haina point

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.