Katika mchezo wa awali wa kundi A hapo jana jioni ilishuhudia Tusker ikipata ushhndi huo wa gol 1-0, goli likifungwa na Jesre Were katika dakika ya 23.
Katika mchezo wa piki wa kukamilisha ratiba hapo jana usiku ulishuhudia Simba sc ikimpatia zawadi ya point moja Bandari baada ya kwenda sare ya kufungana goli 1-1.
Katika mchezo huo Bandari walikuwa wa mwanzo kupata goli kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Haliham Juma katika dakika ya 6, baada ya Haruna Shamte kumkwatua mchezaji wa bandari katika eneo la hatari.
Kiggi Makasi aliyechezeshwa nafasi ya beki wa kushoto ndiye aliyeisawazishia Simba katika dakika ya 16 na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Kwa matfkeo hayo ya michezo ya mwisho ya kundi A hapo jana, Jamhuri na Bamdari wametolewa katika mashindano wakati Simba na Tusker zikitinga nusu fainali. Tusker akiongoza kundi kwa kuwa na point 7 na Simba wakiwafuata wakiwa na point 5, jamhuri akivuna point 3 wakati bandari akiambukia moja.
0 comments:
Post a Comment