TFF

Waamuzi wa ligi kuu watajwa

Waamuzi watakao chezesha michezo ya ligi kuu Tanzania bara watajwa. Kwa mujibu wa taarifa ya afisa habari wa mpira wa miguu TFF Boniface Wambura, majina hayo ni:

Waamuzi wa kati (centre referees).
Ronald Swai (Arusha), Isihaka Shirikisho (Tanga), Peter Mujaya (Mwanza), Amon Paul (Mara), Mathew Akrama (Mwanza), Ibrahim Kidiwa (Tanga), Dominic Nyamisana (Dodoma), David Paul (Mtwara), Hashim Abdallah (Dar), Martin Saanya (Morogoro), Orden Mbaga (Dar), Kennedy Mapunda (Dar), Israel Mujuni (Dar), Alex Mahagi (Mwanza), Abdallah Kambuzi (Shinyanga) na Thomas Mkombozi (Kilimanjaro).

Waamuzi wasaidizi (assistant referees).
walioteuliwa kuchezesha ligi ni 34. Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wa akiba walioteuliwa ni kumi. Hivyo jumla ya waamuzi watakaotumika kwenye ligi hiyo ni 50.

MAKAMISHNA WA MECHI.
Jumla ya makamishna (match commissioners) 24 wameteuliwa kusimamia mechi za ligi hiyo. Kati ya hao 20 ni wa zamani na wanne ni wapya. Makamishna wapya ni Charles Ndagala, Victor Mwandike, Godbless Kimaro na Hamis Tika.

Makamishna wa msimu uliopita walioteuliwa tena ni Hamis Kissiwa, David Lugenge, Abdallah Mitole, Charles Komba, George Komba, Jimmy Lengwe, Amri Kiula, James Mhagama, Fulgence Novatus, Pius Mashera, Michael Bundara, Gabriel Gunda, Mohamed Nyange, Mwijage Rugakingira, Arthur Mambeta, Paul Opiyo, Edward Hiza, Salim Singano, William Chibura na Omary Mwamela.

Uteuzi wa makamishna kama ilivyo kwa waamuzi ulifanyika baada ya kuhudhuria kozi na kufanya mitihani.

Kwa upande wa makamishna ambao hawakufanya vizuri, watalazimika kurudia mitihani kabla ya kuteuliwa tena.

NAULI KWA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI
Kila timu inayoshiriki ligi itapata jumla ya sh. milioni 26.3. Fedha hizo zitatolewa kwa awamu tano tofauti kuanzia mwezi huu. Agosti kila timu itapata sh. 4,732,142, Septemba (sh. 4,732,142), Oktoba (sh. 5,622,321), Januari (sh. 5,622,321) na Machi (sh. 5,622,321).

Jumla ya fedha kutoka kwa mdhamini wa ligi, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambazo zitatumika kwa ajili ya nauli kwa timu zote katika msimu mzima ni sh. 368,637,458.

Boniface Wambura

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.