Mwisho wa jumaa hili kutakuwa na mwendelezo wa mbio za kusaka ubingwa wa Tanzania Bara, pamoja na mbio za Tabora Maradhoni.
JUMAMOSI machi 10.
TABORA.
Kesho kutakuwa na mbio za Tabora Maradhon zitakazo anza saa mbili na nusu asubuhi katika mkoa wa Tabora. Mbio hizo zinataraji kushirikisha wanariadha 300.
DAR ES SALAAM
Katika uwanja wa Taifa kutakuwa na mpambano wa wiki kati ya Yanga na Azam FC. Mchezo huo utawakutanisha washambuliaji wawili wanao wania ufungaji bora ambao ni John Bocco mwenye magoli 13 na Kenneth Asamoah mwenye magoli 10.
Yanga ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu, na mchezo huo watautumia kutaka kurejea katika nafasi ya pili na kuendelea kumfukuzia mpinzani wake wa jadi Simba SC.
Yanga na Azam wamekutana mara 3 msimu huu, ambapo walikutana katika duru la kwanza na Yanga kulala goli 1, mchezo wa pili ulikuwa wakirafiki na kufungwa goli 2. Na mara ya mwisho ilikuwa katika Kombe la Mapinduzi ambapo Yanga walilala kwa goli 3-0.
Mara ya mwisho kwa Yanga kuifunga Azam ulikuwa mchezo wa kuwania nafasi ya pili na kuendelea kuivukuza Simba katika msimu wa 2010/11 ambapo Yanga walishinda kwa goli 2-1 magoli yote ya Yanga na Jerry Tegete na Yanga kuwa bingwa katika msimu huo.
Wakati yanga wakiwa na dhamira ya kulipa kisasi kwa Azam na kufunika jeraha walilo lipata katika mchezo dhidi ya Zamalek wiki iliyopita, Azam FC watakuwa na dhamira ya kuongeza pengo baina yao na Azam kutoka point 1 mpaka 4 na kujiweka sawa katika safari ya kutimiza lengo lao lililo shindwa kutimizwa msimu uliopita.
JUMAPILI machi 11
DAR ES SALAAM
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba SC watawakaribisha Toto Africa ya Mwanza katika uwanja wa Taifa katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Toto Africa wamekuwa na wakati mgumu katika mzunguko wa pili na mpaka sasa hawajashinda mchezo wowote ule zaidi ya sare na kufungwa katika duru hili.
Simba SC huenda katika mchezo huo wakamkosa Mwinyi Kazimoto na mshambuliaji wake hatari toka Uganda Emanuel Okwi walio majeruhi katika mchezo huo.
DODOMA
Katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma kutakuwa na mpambano wa ligi kuu ya vodacom kati ya Kagera Sugar na Polisi Dodoma.
Polisi wamekuwa na wakati mgumu kila wanapoteremka katika uwanja huo, ambao anautumia kama uwanja wake wa Nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment