
Akizungumza na waandishi habari, mkuu wa kitengo cha habari na mausiano Jerry Muro alisema kuwa "Tumefikia uamuzi wa kuachana na Kaseja, baada ya yeye mwenyewe kuanza kujiengua katika timu".
Kaseja alijiunga na yanga mwishoni mwa mwaka juzi na kuidakia yanga katika michezo 15 kabla ya kuwasilisha barua kwa mwajiri wake, Yanga SC kutoa taarifa ya kuvunja makataba wake, uliokuwa umebakiza mwaka mmoja.
Kaseja alipata kunukuliwa akisema kuwa sababu ya kuvunjwa Mkataba huo ni kukiukwa kwa masharti yaliyokubaliwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Novemba 8, mwaka juzi.
Mwakilishi wa Juma Kaseja amenukuliwa akisema wakati wa kusainiwa Mkataba huo ilikubaliwa malipo ya Sh. Milioni 40 yafanyike kwa awamu mbili, awamu ya kwanza, alipwe Sh. Milioni 20 baada ya kusaini Mkataba huo, na ikakubaliwa fungu lililobaki apatiwe Janauri 15, mwaka jana na kwa sababu malipo ya fedha ndio msingi wa Mkataba wenyewe, kushindwa kulipa fedha hizo kunaondoa uhalali wake.
0 comments:
Post a Comment