Ningependa kufungua mjadala huu kwa mesage yangu kwa mchambuzi wa soka mashuhuri nchini Shaffih K Dauda niliyomuandikia september 9 2010, ambayo inasema;
"Mchezaji anaeongoza kuifungia taifa star mabao na idadi ya mabao. Mchezaji alieichezea taifa star mechi nyingi. Mfungaji bora wa wakati wote simba na yanga pamoja na ligi kuu bara. Hizo takwimu zikiwekwa wazi zinaweza kuamsha ari ya kina Ngassa.
Tunaona namna Villa na Klose wanavyopigana kuweka rikodi kwenye mataifa yao. nimechoka kuckia yule forwad alikuwa noma pale anapostaafu."
Ndugu yangu Alex Mkelemi baada ya kusikiliza sports xtra jana akaweka post kwenye Kandanda inayosema;
"Jana nilikuwa nikisikiliza kipindi cha michezo cha Sports Xtra cha Radio ya Clouds. Kuna msikilizaji alituma sms na kuwauliza Shaffi na waliokuwa wakiongoza kipindi hicho. Msikilizaji alitaka kujua ni mchezaji gani mwenye umri mdogo kabisa ambaye amewahi kuchezea timu ya taifa!
Kimsingi kina Shaffii hawakuwa na jibu la moja kwa moja zaidi ya kudonyoa huku na huku wakijaribu kubahatisha. Swali hili kwangu mimi lilizua hisia kali sana.
Nikajiuliza hivi leo ukienda pale TFF wanaweza kukwambia Marehemu Gibson Sembuli aliifungia magoli mangapi timu ya Taifa wakati akichezea. Hivi TFF wanazo takwimu zinazoonesha Abdallah Kibaden alicheza mechi ngapi kwenye timu ya Taifa!
TFF wanawezaje kupanga mipango ya maendeleo ya soka kama hawana takwimu mbali mbali za soka letu. Watajuaje Mbwana Samatta anacheza vizuri zaidi ya alivyokuwa anacheza Sunday Manara kama hawana takwimu za Sunday Manara.
Juzi hapa kuna mtu alikuja na hoja ambayo aliuliza mchezaji gani anastahili heshima ya kujengewa sanamu kwa mchango wake katika soka. Angalia tulivyojigonga gonga humu kwa hoja za kutoka vichwani mwetu tu. Sikuona hata mtu mmoja aliyekuja na ‘reference’. Juzi nilikuwa naangalia tovuti ya NBA. Wana kumbukumbu ya zaidi ya miaka 100 iliyopita! Ukitaka kumtofautisha Michael Jordan na Karim Abdul Jabar huna haja ya kubahatisha kila kitu kipo pale.
Nawasihi sana TFF waanze mpango wa ku- archive kumbukumbu muhimu sana za soka ili tuweze kujua muelekeo wetu bila hivyo tutaendelea ‘kung’ong’ana’ tu!"
MWISHO WA NUKUU
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment